R.I.P. Ustaz Haroub Othman (BBC Swahili)
Inna lillahi wa ina alahi rajioun
Profesa Othman, ambaye amekuwa mchambuzi wa maswala mbali mbali kwenye matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC, alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kwa zaidi ya miongo mitatu.
Kwa wengi anaeleweka kuwa ni mchambuzi wa masuala ya siasa, uhusiano wa kimataifa na mambo ya maendeleo.
Majukumu
Mwanazuoni huyo amekuwa mwenyekiti wa Kituo cha Sheria cha Zanzibar, jukwaa ambalo lilimpatia fursa ya kuzungumzia mambo mengi kuhusu demokrasia, utawala bora na sheria huko Zanzibar.
Wakati anafariki pia alikuwa ni mjumbe wa Baraza la Habari la Tanzania na katika uhai wake ametumikia tume mbali mbali za kiserikali ikiwemo ile ya Jaji ya Nyalali ambayo ndio ilioifungulia Tanzania milango ya kuwa na siasa za ushindani wa vyama hapo 1992.
Profesa Othman alipata elimu yake ya juu huko Urusi na Chuo Kikuu cha Dar es salam na alikuwa ni mwanaharakati aliyehimiza Umoja wa Afrika na kuwa karibu na wana harakati wa zama za kujikomboa na wenye fikra za kizazi kipya kote barani Afrika na duniani.
0 comments:
Post a Comment