March 11, 2009

Nipo Zanzibar Tena







Tangu kufika nilikuwepo kazi nyingi sana. Juzi mchana, nilifika nikaendelea moja kwa moja hotelini yangu karibu na bandhari ipo eneo la Malindi. Kiangazi niliikumbuka na nikaweza kupata bei rahisi mara hii kwa sababu kipindwi isiyo watalii. Usiku ile nilimkutana kijana alisema anionyeshe sherehe ya Reggae. Nilienda naye, tulikuwepo sherehe moja halafu tulienda disco pia. Takriban saa tisa na nusu alfajiri tuliondoka sherehe na tulipotembea kwangu (alifuatana nami). Alipiga magoti ili kushika mawe makubwa halafu alisimama akisema (kwa Kiingereza): Nipe kila kitu...pesa...nahitaji pesa ili kununua dawa kulevya. Nilimwambia: wewe unapayuka! Akapanza mawe juu ya kichwa yake kama akinipiga na akapaaza sauti akisema: nipe ninacho! Kweli nimeshangaa kwanza nafikiri huyu anafanya mzaha tu lakini alikuwa hatari kwa hivyo nilianguka na nikatoroka. Alhumdullilah, hakufuata nami.

Siku pili, nililala sana baadaye nikasoma pia ili kujitayarisha kwenda nyaraka za taifa. Nilienda Jumatatu asubuhi. Nilipofika ofisini ya nyaraka. Bibi katibu aliyepo nyuma ya meza alisema kwamba walipokea maombi yangu lakini bado hawaijapeleka wizara na mkurugenzi ya nyaraka alikuwepo Pemba hawezi kupokea phone calls. Baada ya mazungumzo mrefu na katibu mwingine, walisema kwamba nipo ruhusa kuingia tu na kuangalia tu, mpaka kesho kutwa wakati walipokea ruhusa mwisho kutoka wizara.

Nimefurahi sana kuangalia tu.

Leo sikukuu ya serikali kwa hivyo nilichagua kwenda Mkokotoni ili kupanda boati nikiendesha kisiwa cha Tumbatu. Njiani mvua ilianza kutoka kali sana kwa hivyo tulipofika Mkokotoni nilichagua tena kurudi kwangu wakati abiria moja aliniambia aende Nyungwi ipo kaskazini kabisa. Tulienda pamoja kwa daladala. Tukifika tulitembea tembea mpaka mwanzo kazi ya mwenzangu. Anaitwa Eriena. Yeye Mkristo anatoka Dar es Salaam, ana ndugu tano, dada mbili na kaka tatu mdogo. Aliwajua watu wote akicheka na akizungumza nao. Tulikula pamoja na nilizungumza na mtu mwingine akijua Kiarabu.

Mambo yangu ya afadhali yalikuwa nilipopanda basi ya wafanyakazi kutoka Nyungwi kwenda Mji Mkongwe. Wote wanaambiana masihara. Kwa mfano: mtu moja hamna nyumba kwa hivyo hawa walimchokoza: "eh bwana, wageni wako wakaaje?" Kila mara iliposemekana ilituchekesha!

0 comments:

  © Blogger templates The Professional Template by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP